Alhamisi 27 Novemba 2025 - 12:55
Mashia Nchini Kenya Waadhimisha Kumbukumbu ya Shahada ya Bibi Fatma Zahra (as)

Hawza/ Kufuatia na kuadhimisha masiku ambayo yanasadifiana na siku aliyopata shada Binti wa Mtume, Bibi Zahraa (as) Mashia nchini Kenya nao pia waliadhimisha tukio hilo la kuhuzunisha.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Mshauri wa Masuala ya Utamaduni wa Iran jijini Nairobi, Dkt. Mehdi Beigi, aliungana na Mashia wenyeji nchini Kenya katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuuawa kishahidi kwa Fatma Zahra, binti wa Nabii Muhammad (Rehema na Amani ziwe juu yake na Aali zake).

Hafla hiyo ya huzuni na mawaidha iliambatana na hotuba iliyotelewa na Hujjatul Islam Sheikh Juma Shughuli, ambaye alielezea kwa kina nafasi ya Bibi Zahra (as) katika historia ya Uislamu na umuhimu wa msiba wa shahada yake katika kujenga misingi ya itikadi, subira na kusimama katika haki.

Sheikh Juma Shughuli alisisitiza kuwa kifo cha kishahidi cha Bibi Zahra (as), kinachukuliwa kuwa ni moja ya misiba mizito na ya msingi kabisa katika ulimwengu wa Kiislamu, kwa kuwa kinahusishwa moja kwa moja na dhulma aliyofanyiwa baada ya kufariki Mtume Muhammad (saww). Alifafanua kuwa shahada hiyo ilitokana na majeraha aliyoyapata wakati wa kushambuliwa nyumba yake muda mfupi baada ya kifo cha baba yake.

Kwa mujibu wa simulizi za Kishia, shambulio hilo lilihusisha kuchomwa moto kwa nyumba hiyo na kuvamiwa kwa nguvu, jambo lililosababisha mimba ya mwanawe aliyeitwa Muhsin kuharibika, na hatimaye akafariki dunia kati ya siku 75 hadi 95 baada ya kufariki baba yake, Mtume Muhammad (saww).

Katika hafla hiyo, waumini walihimizwa kuyaenzi mafunzo ya Fatma Zahra (as) ya subira, ucha-Mungu, uadilifu na kusimama upande wa haki, huku wakikumbushwa kuwa kumbukumbu hizi si za huzuni pekee, bali ni dira ya kuijenga jamii yenye misingi ya maadili na haki.

Mashia Nchini Kenya Waadhimisha Kumbukumbu ya Shahada ya Bibi Fatma Zahra (as)

Mashia Nchini Kenya Waadhimisha Kumbukumbu ya Shahada ya Bibi Fatma Zahra (as)

Mashia Nchini Kenya Waadhimisha Kumbukumbu ya Shahada ya Bibi Fatma Zahra (as)

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha